KIKAO KAZI
Manispaa ya Ubungo leo tarehe 17 Mei ,2022 imepokea ugeni kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -Tamisemi na wadau wa Mnyororo wa Ugavi na Usambazaji ambao walifika kuona utekelezaji wa mkakati wa Impact Team ambao unalenga kutumia takwimu za bidhaa za afya katika kufanya maamuzi kama timu yenye lengo la kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya katika Vituo vya kutolea huduma za afya.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Mfamasia wa Manispaa ya Ubungo Bi. Doris Mollel amezungumzia kuwa ujio wa ugeni huo ambao umeleta manufaa katika kuwajengea uwezo zaidi wataalamu wa afya katika kuboresha takwimu za bidhaa za afya sambamba na kutoa elimu ambayo impact team Manispaa ya Ubungo inaenda kuifanyia kazi
"Mbinu ya Impact Team imetusaidia kwa kiwango kikubwa kukabiliana na changamoto mbalimbali za takwimu za bidhaa za afya na hivyo kuongeza kiwango cha dawa katika vituo vyetu lakini pia tumepokea elimu ambayo itaenda kutupa mwelekeo katika kuweka mbinu zaidi ambazo zitaenda kukabili changamoto ya bidhaa za Afya kwa kuhakikisha zinapatikana muda wote katika vituo vya kutolea huduma. Alieleza Doris
Aidha, Ndg.Deus James Mfamasia na mwezeshaji wa Impact Team Approach wa kitaifa amewapongeza watumishi wa Idara ya Afya kupitia Impact team kwa kazi kubwa wanayofanya na kuwaaasa waendelee kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha uendeshaji wa mfumo wa Bidhaa za Afya katika Vituo unafanyika vizuri.
Nae Ondo Baraka mdau kutoka USA Global Health ambaye anafanya kazi na Wizara ya Afya katika kusaidia mifumo ya ugavi na usambazaji wa bidhaa za afya amezungumzia swala la ufuatiliaji wa afua za mnyororo wa ugavi na usambazaji wa bidhaa za Afya katika Vituo na katika eneo zima la kuchakata Data kuwa ni suala endelevu na linalotakiwa kupewa kipaumbele ili kuhakikisha wateja wanapata dawa muda wote.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa