Mratibu wa bima ya iCHF Ubungo Leticia Meena jana tarehe 18/03/2022 ametoa elimu ya bima ya iCHF kwa wafanyakazi wa kampuni ya Rafael Logistics iliyopo Kata ya Makuburi lengo ikiwa ni kuwezesha wafanyakazi hao kuwa na uhakika wa matibabu kwa kuwa na bima ya iCHF.
Meena ameeleza kuwa bima hiyo ipatikana kwa Tsh 150,000/= kwa familia ya watu sita na Tsh 40,000/= kwa mtu mmoja ambapo mteja wa bima hiyo atapata huduma kwa utaratibu wa rufaa kwa kuanzia zahanati, kituo cha afya na hospitali za rufaa za Mkoa za Serikali. Kwa sasa mteja anaweza kuanzia kituo cha afya moja kwa moja.
Aidha Meena ameeleza mteja wa bima ya iCHF anahaki sawa na mteja mwengine yeyote wa bima yeyote hivyo mteja huyo anapaswa kupata huduma zote zinazotelewa zahanati, kituo cha afya na hospitali za rufaa bila kama utaratibu unavyotaka na endapo dawa zitaisha mahali ambapo mteja anapata huduma basi daktari anapaswa kuwasiliana na mahali pengine pa huduma ili mgonjwa/ mteja huyo akapate huduma hiyo bila yakumlipisha fedha yoyote.
Baada ya elimu hiyo walipatikana wafanyakazi zaidi ya thelathini ambao waliahidi kukata bima hiyo na kwamba walionesha kufurahishwa kwa uwepo wa bima hizo kwani zitaenda kusaidia kupata uhakika wa matibabu kwao na kwa wategemezi wao na kuondoa msongo wa mawazo pindi wanapopata magonjwa mbalimbali.
“Ugonjwa hauna taarifa mara nyingi tunapoumwa kuna muda huwa tunakosa hata fedha tu ya kwenda kujua tunachoumwa lakini ukiwa na bima hakuna mawazo tena kwani tayari unakuwa na uhakika wa matibabu kata bima ya iCHF kwa maslahi mapana ya afya yako afya ni mtaji”. Alisema Meena.
Kwa upande wake Dkt Hashim Limira amewahasa wafanyakazi kuchanja chanjo ya UVIKO 19 ili kuendelea kujikinga na ugonjwa huu ili kuweza kuutokomeza.
“Akichanja kila mtu sote tutakuwa salama UVIKO 19 itabaki kuwa historia”. Alisema Limira.
Katika kuendelea kuhamasisha timu ya uhamasishaji aliyoongozana nayo Meena ilifanikiwa kupita Kata ya Manzese nyumba kwa nyumba ili kuelimisha wananchi juu ya chanjo ya UVIKO - 19 ambapo pia walifanikiwa kuchanja wananchi katika siku hiyo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa