Ikiwa imebaki mwezi moja na nusu kumaliza mwaka wa fedha wa 2020/2021, Manispaa ya Ubungo imeweka mkakati wa kuongeza ukusanyaji wa Mapato Kwa kuwafikia wateja kwenye maeneo yao pamoja kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa tozo mbalimbali kwa hiari ili kufikia asilimia 100 ya makusanyo
Mpango huo umetolewa leo na mkurugenzi wa manispaa ya ubungo Beatrice Dominic kwenye kikao kilichohusisha wataalam wa ukusanya wa mapato na vyanzo mbalimbali vya Halmashauri na kueleza kuwa hadi sasa halmashauri makusanyo yamefikia 86℅ hivyo tumebakiza 16 ℅ kufikia lengo la asilimia 100
"Nawapongeza kwa kazi kubwa mnayofanya kwani kufikia asilimia 86 nikazi kubwa mmefanya nawaomba muongeze bidii yakuwafikia wateja wetu ambao hawajilipa kodi na tozo mbalimbali ilitufikie asilimia 100 ifikapo juni 30 mwaka huu" alieleza Dominic
Aidha alieleza kuwa pamoja na jitihada hizo Halmashauri imejipanga kufikia mkakati wake wa kuwafikia wateja wake kwenye kata ikiwa ni sehemu ya kuwasogezea huduma za kulipia tozo na huduma zingine hivi karibuni
Aidha mkurugenzi anawasisitiza na kuwataka wananchi wote kulipia leseni zao za biashara na tozo za halamashauri kuwezesha maendeleo ya Halmashauri ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa, vityo vya afya, madawati na miunfombinu mingine ambayo inawagusa wananchi moja kwa moja
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa