Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa LAPAZ uliopo Luguruni na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic na kuhudhuriwa na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dkt.Peter J.Nsanya, Mwenyekiti wa bodi ya afya Manispaa ya Ubungo Ndg.Israel Sosteness na Wataalam kutoka katika Manispaa ya Ubungo.
Katika uzinduzi huo kamati zilielekezwa majukumu yao ambayo ni kusimamia vituo kwa shughuli za kila siku, kusimamia maboresho ili wanachi wapate huduma bora za Afya ,matumizi ya dawa, kushiriki katika mipango ya kituo kila mwaka,Wajumbe hao pia wamefundishwa juu ya ukaguzi wa dawa vituoni(drug audit) n.k
Aidha Mkurugenzi aliongea Kamati zote za Afya Manispaa ya Ubungo kutoka zahanati,Vituo vya Afya na Hospitali juu ya Ukaguzi wa dawa kwenye Vituo hayo , iCHF ianze na wao poa jamii inayowazunguka, Vilevile aliwapongeza wataalam wote ambao wapo kwenye vituo kwa kufanya kazi vizuri na kutoa huduma nzuri mfano kituo cha Afya cha Sinza, Kimara, Mbezi n.k
"Niwaase wajumbe mkapate huduma katika zahanati na vituo vya afya vilivyopo katika Manispaa ya Ubungo ili kuongeza mapato". aliongeza Mkurugenzi
Vilevile aliwakabidhi miongozo wajumbe wa Kamati ya Afya zahanati ya malamba mawili na wajumbe wa kamati ya Afya Hospitali ya Sinza.
Nitamke rasmi kamati ya sinza na malamba mawili imezinduliwa rasmi leo tarehe 12/9/2020
Aidha Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo *Dkt.Peter J. Nsanya* aliwataka wajumbe kuwa mawakala wazuri wa kushawishi wananchi wa wilaya ya Ubungo kujiunga na bima ya Afya ya Jamii (ICHF) ili kupata huduma za afya kwa gharama nafuu.
"ICHF ni bima inayomsaidia mwananchi yoyote wa hali ya chini kupata huduma ya matibabu kwa gharama ya Tsh40,000 kwa mtu mmoja na 150,000/=kwa familia ya watu sita baba, mama na tegemezi wake wanne kwa mwaka mzima" aliongeza Mganga Mkuu.
Sambamba na hayo Mganga Mkuu aliendelea kuwakumbusha wajumbe kuwa ni muhimu wakatambua majukumu yao na kuzingatia misingi ya kazi zao.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Manispaa ya Ubungo *Ndg.Sostenes Israel* aliwashukuru wajumbe wa kamati na kuwasihi kuzingatia majukumu yao na kuwapongeza kwa kazi nzuri ambazo zinafanyika.
Mwisho Mkurugenzi aliwashukuru wajumbe kwa ujio wao na kuwapongeza kwa kujitokeza kwa wingi pia aliwaasa wakafanye kazi ipasavyo na kuwataka wakajitokeza kwa wingi wakati wa uchaguzi iliwaweze kuchagua viongozi wao.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa