Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imezindua muongozo mitatu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Elimu ambayo utasaidia kuleta mageuzi chanya katika usimamizi wa elimu na kuongeza tija katika ufundishaji mashuleni
Uzinduzi huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kutaka Miongozo hiyo izinduliwe ngazi ya Wilaya pamoja na kuizindua ngazi ya Taifa ili kuleta uelewa na ufanisi katika utekelezaji wa miongozo hiyo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James amewapongeza Walimu wa Manispaa hiyo kwa utumishi bora kwenye kazi zao za kila siku za kuwafundisha wanafunzi pamoja na kuwalea wanafunzi katika maadili bora ya kitanzania.
"Mwalimu ni mtu pekee anayekutana na watoto wa aina zote kila siku hivyo ana nafasi kubwa ya kuwajenga katika misingi iliyo bora kitaaluma na kijamii kwani pamoja kuwapa elimu lakini pia ni mlezi" alieleza Mhe. James
Aidha, amewataka walimu kubuni mbinu nzuri zitakazosaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi kwa kushirikiana na wazazi na walezi ili kuwa na makubaliano ya pamoja na kuepusha malalamiko.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic amesema kuwa kupitia miongozo hiyo ambayo imezinduliwa leo itaenda kuleta tija kubwa kwenye sekta ya elimu na itawafanya walimu wajisikie fahari kufanya kazi yao
Pia, Beatrice amesema kuwa Manispaa ya Ubungo imeshapokea fedha jumla ya shilingi Bilioni 1.6 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 81 ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023
Ametumia nafasi hiyo kuwasihi walimu watakaopata fedha za ujenzi wa madarasa kutekeleza miradi hiyo kwa wakati na ubora ili watoto wote watakaofaulu kujiunga kidato cha kwanza kuanza masomo kwa wakati na kwenye mazingira bora.
Miongozo hiyo iliyozinduliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Mkoani Tabora ni pamoja na mwongozo wa uteuzi wa viongozi wa elimu, mwongozo wa mkakati wa ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya elimu msingi na mwongozo wa changamoto katika uboreshaji wa elimu msingi na sekondari
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa