Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kibamba na Ubungo Beatrice Dominic Leo tarehe 21 oktoba, 2020 amewaapisha Mawakala wa vyama mbalimbali vya siasa vitakavyoshiriki zoezi la uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika oktoba, 2020.
Akiendesha zoezi Hilo, Beatrice amewataka Mawakala hao kutunza Siri za Uchaguzi Kama walivyoapa kwenye viapo vyao pamoja na kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za Uchaguzi za mwaka 2020 ili zoezi hilo lifanyike kwa amani na utulivu.
"Ni haki ya kila chama cha siasa kinachoshiriki Uchaguzi kuwa na wakala, ila tambueni kuwa Kwa wakala atakayeshindwa kuzingatia kiapo hiki hatua za kisheri zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kulipa faini au kifungo au vyote kwa pamoja" Beatrice alieleza
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi jimbo la Ubungo Kissah Mbilla akiwaapisha mawakala katika kata ya Ubungo Leo tarehe 21 oktoba, 2020
Aidha, Beatrice ameendelea kuwaeleza mawakala hao kuwa, kuapa kiapo hicho ni utekelezaji wa kanuni ya 50(4) ya kanuni za uchaguzi wa Rais na wabunge za mwaka 2020 na kanuni ya 43(4) ya kanuni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa( uchaguzi wa madiwani) za mwaka 2020.
Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi jimbo la Kibamba Tumaini E Mrango akiwaapisha mawakala wa vyama vya siasa katika kata ya Kwembe Leo tarehe 21 oktoba,2020
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa