Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo ambaye pia ni Waziri Ofisi ya Rais Uwekezaji amewahakikishia wananchi wa Jimbo hilo kushughulikia kero zao ikiwemo tatizo la barabara za mitaa, maji, elimu na afya kikamilifu ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake wakati wa kampeni.
Hayo ameyazungumza kwa wananchi wakati alipofanya Ziara ya Siku nne katika kata za Kimara, Manzese, Sinza ,Mabibo na Makulumla kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuweka mikakati ya kuzitatua.
Aidha katika Ziara hiyo Prof. Kitila akipokea taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ya mavulunza na ujenzi wa Hospitali ya Sinza Palestina ambapo amepongeza utekelezaji wake na kuahidi kushirikiana nao kuhakikisha rasilimali fedha inapatikana ili miradi hiyo ikamilike ili wananchi waanze kupata huduma.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof Kitila Mkumbo (alievaa miwani) akiendelea na ziara ya kutambua kero za wananchi kata ya kimara.
Prof Kitila amefafanua kuwa "Kukamilika kwa Miradi hii kutaongeza ustawi wa wananchi mfano ujenzi wa hospitali ya sinza ambayo inahudumia wagonjwa kati ya 800 hadi 1000 kwa siku unapaswa kukamilika kwa haraka ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi wetu"
Prof Kitila ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa kutoa fedha za mapato yake ya ndani zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kupanua ujenzi wa hospitali hiyo huku serikali ikitoa shilingi milioni 200 kutokana na hospitali hiyo hudumia wengi sana watu.
Akitoa taarifa hiyo mbele ya Mhe. Mbunge huyo, mganga Mkuu wa Manispaa Ubungo Peter Nsanya alieleza kuwa, hospitali ya sinza palestina ilipandishwa hadhi kutoka kituo cha afya na kuwa hospitali ya Wilaya mwaka 2016 wakati Manispaa ya Ubungo ilipoanzishwa kikimegwa kutoka Manispaa ya kinondoni.
Aidha Nsanya alisema kuwa kukamilika kwa hospitali hii kutapanua utoaji wa huduma za afya ikiwemo upatikanaji wa huduma za kibingwa ikiwemo upasuaji mkubwa tofauti na sasa ambapo upasuaji unaofanyika ni ya uzazi pekee.
Katika Ziara hiyo Mhe Waziri alitembelea pia maeneo ya mto gide, bonde la mto china, na mto ng'ombe kujionea athari zinazosababishwa na mito hiyo kwa wananchi ikiwemo kubomboa makazi.
Pamoja na kwamba serikali imeendelea kuchukua hatua ya namna ya mito hiyo isiendelee kutela madhara kwa wananchi Prof Kitila amewaomba wananchi kuchukua hatua ikiwemo kuto jenga makazi au kufanya shughuli za kiuchumi karibu na mito ili kupunguza madhara yanayotokea sasa.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof Kitila Mkumbo ambaye pia ni waziri wa Uwekezaji akiongozana na viongozi mbalimbali kukagua athari za mto Ng'ombe
Wakati wa Ziara hiyo, pia Mhe. Waziri alitembelea na kuzindua kazi mbalimbali za sana na michezo ikiwa ni moja ya sekta muhimu inayowaingizia watu kipato hususani vijana na kuwaeleza kuwa sekta hiyo ni nzuri kwani soko lake ni pana sana " hivyo mjitume na mthamini kazi zenu kwani serikali pia inatambua mchango wenu kwa Taifa.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa