Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Mheshimiwa Jaffary Juma Nyaigesha amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Manispaa hiyo Shilingi bilioni 3.02 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 151 kwa Shule za Sekondari ili kumaliza changamoto ya upungufu wa madarasa katika shule za Manispaa hiyo
Ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa utafanikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2022 kupokelewa na kuendelea na masomo katika mazingira mazuri ya kujifunza na kujifunzia.
Mhe. Jaffary ametoa shukrani hizo leo Oktoba 28, 2021 kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za Maendeleo ngazi ya kata na kuwaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa, ujenzi utafanyika kwa kipindi cha miezi miwili ambapo hadi kufikia 15 Desemba, 2021 madarasa hayo yanapaswa yawe yamekamilika na tayari kwa matumizi.
"Kutokana na muda wa utekelezaji wa ujenzi wa madarasa hayo kuwa mfupi, Mstahiki Meya amewaomba waheshimiwa Madiwani na Watendaji wote kusimamia ipasavyo ujenzi wa vyumba ikiwemo kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo katika kutekeleza miradi hiyo.
"Inatupasa tushirikiane kwa hali na mali ili kusiwe na kikwazo chochote kitakacho kwamisha utekelezaji wa miradi hii ukizingatia muda wa utekelezaji ni mfupi sana"
Mgao wa fedha hizo ni kati ya shilingi trilioni 1.3 za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 uliozinduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mwezi Oktoba 10, 2021
Pamoja na kupata fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa 151, pia Halmashauri imepata fedha Shilingi Milioni 420 kwa ajili ya ununuzi wa mashine ya Mionzi ( X-Ray) itakayotumika katika Hospitali ya Wilaya na hivyo kufanya Halmashauri kupata mgao wa Shilingi bilioni 3.44.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa