Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dr. Peter Nsanya ametoa elimu kuhusu ugonjwa wa Corona katika kanisa la KKKT lililopo Sinza siku ya jumapili tarehe 15/3/2020
Dr. Nsanya aliwaelezea waumini hao juu ya sababu za ugonjwa huo na namna ya kujikinga.
"Niwaambie kuwa kirusi hiki kinaweza kukaa kwenye mikono kwa dakika 10, kwenye nguo Massa 9 na kwenye chupa Massa 12" alisema Dr.Mganga Mkuu, pia alieleza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. John Joseph Magufuli na kupitia idara ya Afya tayari wamejiandaa kuukabili ugonjwa huo hivyo wananchi wasiwe na hofu ya aina yoyote ile. Dr. aliwaomba watu wote kujikinga na ugonjwa huu hatari kwa kutokupeana mikono na sehemu zote ambazo watu huingia basi pawekwe maji ya kutiririka ili kila mtu anaeingia hata kanisani anawe mikono.
Mwisho aliwaomba waumini kutoa ushirikiano pale wanapomhisi mtu kuwa na virusi hivyo basi watoe taarifa kwa mamlaka husika. "Hadi sasa kuna nchi zaidi ya 100 ambazo tayari wameathirika na ugonjwa huu na nchi kama Rwanda wanafunga shule na vyuo aliongeza Mganga Mkuu.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa