Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dk.Peter Nsanya ametoa semina kwa watumishi wa ofisi ya Mkurugenzi waliopo makao makuu Luguruni na Ofisi ya Mbezi.
Halmashauri imetoa Millioni 10 kwa ajili ya kuhakikisha inadhibiti korona kwa kununua vifaa na madawa kwa ajili ya kutakasa mikono kwa watumishi na wateja wao. Alisema hayo Mganga Mkuu.
"Vifaa hivyo ni ndoo, madawa(chlorine) na pia sanitizer zitasambazwa kwenye ofisi za mkurugenzi, masoko na stendi za mabasi kwa Manispaa yote ambazo watumishi na wateja watasafisha mikono yao"
Aidha mganga Mkuu alieleza matumizi sahihi ya maji yanayotiririka na sabuni kuwa ni salama na sahihi kwa kujikinga na korona na pia Maji yenye chlorine na sanitizer na aliendelea kwa kusema kuwa mask zitumike kwenye ulazima maana zinavyotumika si sahihi.
"Uvaaji wa Mask unatakiwa kwa wale wagonjwa ambao tayari wameathirika na ugonjwa huo ili kuepusha maambukizi kwa wengine"
Niwakumbushe epukeni mikusanyiko,kukumbatiana, kubusiana na kumbukeni kunawa mikono kwa maji na sabuni.
Mwisho Mganga Mkuu aliwasihi sana pale wanapoona dalili zozote kuhusiana na ugonjwa huo wahakikishe wanafika katika vituo vya afya kwaajili ya kuonana na watalaam wa afya.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa