Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) wameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha huduma na kuinua wananchi kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani
Timu hiyo iliyoongozwa na Mkurugenzi msaidizi wa Serikali za Mitaa TAMISEMI Ndugu Ibrahim Minja ,imetoa pongezi hizo jana Agosti 2, 2021 baada ya kukagua jumla ya miradi 9 ya Maendeleo ambapo miradi 7 ni ujenzi wa miundombinu na miradi 2 ya vikundi vya wajasiriamali yenye thamani ya thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 59 ambapo kati ya Fedha hizo shilingi milioni 300 ni fedha za mapato ya ndani na kusema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ni chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Manispaa hiyo
Timu pia ilisema "Tumeridhishwa na miradi tuliyotembelea iko vizuri, nawapongeza Kwa kuwa na vikundi venye miradi yenye tija ambavyo sio tu kukuza uchumi wao lakini kutumika kama darasa wananchi wasio wanabikindi"
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Mkoani Athuman Mayunga alisema kupitia ukaguzi wa miradi Mkoa utazialika Halmashauri zingine za Mkoa wa Dar Es salaam kuja kujifunza Ubungo hasa kwenye vikundi kuna ubunifu mkubwa Sana hasa kikundi cha Vijana kinachojihusisha na kilimo kinachozalisha funza kwa ajili ya chakula cha mifugo hasa wa samaki.
Akiongea kwa niaba ya timu ya menejimenti, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic alisema Manispaa ina mpango wa kutoa mikopo mikubwa kwa vikundi vyenye miradi mikubwa ili viweze kutengeneza ajira zaidi kupitia miradi yao ya uzalishaji Mali
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa