Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic leo tarehe 6 septemba amefanya kikao kazi na wakuu wa idara na vitengo pamoja na wataalam wa Halmashauri hiyo kusisitiza swala la ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa vyanzo vya mapato ili kuweza kufikia lengo la billioni 27 kabla mwaka wa fedha 2021/2022 kuisha
Beatrice Aliendelea kuwasisitiza kila mtaalam ahakikishe anasimamia vyanzo vilivyopo nakutafuta njia ya kuboresha na kuongeza ukusanya wa mapato
"Tuhakikishe kila mmoja wetu anazingatia hili kwa manufaa ya maendeleo ya Halmashauri yetu, utekelezaji wa Miradi unategemea pesa za makusanyo ambayo kila mmoja wetu anajukumu la kukusanya mapato hayo" alielezea hayo Beatrice
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa