Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic leo tarehe 10 Novemba, 2020, amefanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Manispaa hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 9.7 lengo ikiwa ni kujiridhisha na hali ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Mradi wa ujenzi wa Jengo la utawala Manispaa ya Ubungo ukiwa kwenye hatua za umaliziaji
Beatrice amefanya ukaguzi huo akiwa na wakuu wa idara wa Manispaa hiyo na kuwaeleza watalaam hao kuwa Hali ya utekelezaji wa miradi bado hairidhishi hivyo waongeze kasi ya usimamizi ili miradi hiyo iweze kukamilika Kwa wakati.
"Nadhani mnafahamu kuwa kila mradi una muda maalum wa kukamilisha, kutokamilisha Kwa wakati tunaenda kinyume na maagizo ya Serikali, nawagiza muongeze kasi ya usimamizi" alisisitiza Beatrice
Beatrice amefafanua kuwa , miradi hiyo inatekelezwa Kwa fedha za kutoka Serikali kuu na fedha za mapato ya ndani hivyo ni lazima ikamilike Kwa wakati ili kuboresha huduma kwa wananchi ambayo ndio adhima ya Serikali ya awamu tano
Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya ukiwa kwenye hatua ya upauaji
Aidha, Beatrice ameendelea kueleza kuwa, mradi wa ujenzi wa standi ya daladala Mloganzira pamoja na kuwasaidia wananchi wanaotumia hospitali ya Mloganzira lakini pia ni chanzo cha mapato Kwa Manispaa, hivyo ni muhimu kuikamilisha kwa wakati ili ianze kutumika.
Akiongea kwa niaba ya watalaam wa Manispaa hiyo warioshirizi ukaguzi wa miradi, Mhandisi wa Ujenzi wa Manispaa hiyo ndugu Juma S Magotto ameahidi kuongeza kasi ya usimamizi wa miradi hiyo ikiwemo kuzingatia ubora wa majengo hayo.
Miradi iliyotembelewa ni ya sekta za Elimu , Afya na Utawala ikiwemo ujenzi wa stendi ya daladala Mloganzila, Ujenzi wa Jengo la utawala na Ujenzi wa hospitali ya Wilaya, ujenzi wa hospitali Sinza, ujenzi wa vyumba vya madarasa 8, vyoo matundu 10, ujenzi wa hosteli shule ya Sekondari Goba pamoja na ujenzi wa mabanda ya soko la wajasiriamali wadogo mbezi.
Mradi wa ujenzi wa standi ya Daladala Mloganzira
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa