Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic leo ametembelea soko la Mburahati kujionea maendeleo yake. Katika ziara yake hiyo Mkurugenzi aliambatana na baadhi ya wataalam kutoka Manispaa hiyo. Soko hili lilijengwa kwa ufadhili wa fedha kutoka Serikali ya Denimark ambayo ilitoa kiasi cha Tshs. Bilioni 1.2. Fedha hizo zilisimamiwa na TGT YAANI (Tanzania Growth Trust) na Vibindo ambazo hazikutosha na kusababisha mradi kusimama kwa takriban miaka miwili. Wakati huo Manispaa ya Kinondoni ilitafuta fedha kutoka vyanzo mbali mbali bila mafanikio.
Aidha Manispaa ya Ubungo ilipata bahati ya kupata fedha ya mradi mkakati mwaka 2018 jumla ya Tshs. Milioni 996 kwa ajili ya kukamilisha mradi huo. Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ndiyo inayosimamia soko hili tangu mwanzo kwenye shughuli zote za uendeshaji. Mkurugenzi alisema kuwa awamu ya pili ya ujenzi huo unahusisha jengo la mama lishe na vyoo na kuwa Mkandarasi aliyepatikana ni SUMA JKT.
Vile vile Mkurugenzi aliishukuru Serikali kwani tayari fedha za ujenzi wa awamu ya pili. zimepokelewa na muda si mrefu ujenzi utaanza. "Nimesikitishwa sana na kauli niliyoisikia hapo jana kuhusu Vibindo kwamba ndio waliohusika na ujenzi wa soko hili pamoja na wadau, kauli hiyo in ukakasi na upotoshwaji kwani Vibindo alidiriki kupotosha ukweli kuwa serikali imetoa Milioni 300 tuu." Alifafanua Mkurugenzi.
Beatrice alimaliza kwa kusema kwamba soko la Mburahati ni moja kati ya orodha ya miradi ya kimkakati ambayo inatekelezwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusimamiwa na Manispaa ya Ubungo. Aliwaasa awafanyabiashara kutunza miundombinu ya soko ili kuenzi kazi kubwa inayofanywa na Serikali yetu.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa