Tarehe 23/5/2020 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo alitembelea katika kituo cha watoto yatima cha IJANGO ORPHANAGE CENTER kilichopo Kata ya Sinza na kuhudhuliwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic, Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Ubungo wakuu wa Idara na vitengo na Jumuiya ya Wazazi kata ya Sinza.
Wakati wa tukio hilo Mkurugenzi alitoa pongezi kwa mlezi wa kituo hicho na kumshukuru kwa juhudi alizofanya kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yao na malezi kwa ujumla.
Aidha mkurugenzi alimkabidhi vitu vilivyonunuliwa ikiwa ni pamoja na vyakula ( mchele,nyama, maharage,mafuta ,unga, sabuni, sanitizer n.k) na kumkabidhi Tsh160,000 kwa ajili ya kununulia mahitaji mengine kwa ajili ya sikukuu ya Idd
Sambamba na hilo alihaidi kupeleka gari la Manispaa la kunyonya maji taka yanayotoka chooni na pia kuahaidi kuendelea kushirikiana nae bega kwa bega kuhakikisha wanawaisadia watoto hao.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dk.Peter Nsanya aliwahaidi kuhakikisha watoto hao wanakatiwa bima ambayo itawasaidia kupata matibabu.
Nae mlezi wa watoto hao Bi. *Nuru Hassan* aliwashukuru kwa ujio huo na kwa vitu ambavyo mmevileta kwa watoto hawa ambao ni yatima ambao wanahitaji kufarijiwa hakika mmesaidia kwa mchango mkubwa na niwakaribishe mara kwa mara kuja kuwatembelea na kuona maendeleo ya watoto hawa.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa