Kikao hivho kilifanyika katika ukumbi uliopo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Luguruni huku lengo kuu ni kufikia mwafaka juu ya bei ya kulipia kwenye vibanda vya masoko.
Kikao hicho kimeongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic na kuhudhuriwa na Mwanasheria wa Manispaa Kissah Mbilla Afisa Biashara, Prisca Mjema na viongozi wa masoko hayo na baadhi ya wataalam.
Lengo kuu la kikao hicho ni kukubaliana juu ya gharama ambayo wapangaji wa vibanda ambao ndio wajenzi wa vibanda hivyo watapaswa kulipia kwa Halmashauri.
Katika kikao hicho Halmashauri na wapangaji walikubaliana kuunda timu ya watu wachache ambao watapita kila kibanda kwa masoko yote kwa siku mbili na kupanga bei ambayo Halmashauri na wapangaji watakuwa wamekubaliana.
Baada ya makubaliano ya bei kila mpangaji atatakiwa kulipa madeni yote ya nyuma na malipo ya miezi miwili ya bei mpya na kusaini Mkataba na Halmashauri
Vile vile wamekubaliana kuwa siku ya mwisho ya kusaini mkataba huo itakuwa tarehe 30/05 na kikao kwa ajili ya kufanya maamuzi kwa wale ambao watakuwa hawajalipa madeni na kusaini Mkataba kitafanyika tarehe 03/06
Baada ya makubaliano hayo Mkurugenzi aliwashukuru viongozi hao wa masoko ya Sinza na Shekilango kwa kuitikia wito na kuwaahidi ushirikiano wa kutosha na kuwaomba wao pia kushirikiana na timu ya wataalam watakaofanya nao kazi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa