Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic amepokea darasa moja kwa ajili ya watoto wanaosoma darasa la awali kutoka Shirika la OCODE (ORGANIZATION FOR COMMUNITY DEVELOPMENT) katika Shule ya Msingi Kibwegere iliyopo kata ya Kibamba.
Shirika hilo la OCODE pia limetoa madawati 38 na viti vya walimu 13 yote hiyo ni kuisaidia Serikali kuletea maendeleo wananchi.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Shirika hilo Ndg. Joseph Jackson alisema mradi huu ndio wa kwanza kwao kuzindua. *”Niseme wazi huwa hatuna desturi ya kuzindua miradi tunayoitoa kwa Halmashauri au wananchi na hii ni mara ya kwanza”* alisema Ndg. Jackson.
Aliongeza kuwa kwa sasa Shirika lina miradi minne katika kata tatu za Manispaa ya Ubungo ambazo ni Kibamba, Goba na Msigani katika maeneo ya Kibwegere, Kiluvya, Goba na Malamba Mawili. ”Nikutaarifu tu Mkurugenzi kuwa hadi sasa chumba cha darasa kama hiki tayari kimeanza kujengwa Goba.” aliongeza Mkurugenzi wa Shirika.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo alimshukuru Mkurugenzi wa Shirika la OCODE na Shirika lote kwa ujumla kwa msaada wanoutoa katika kuhakikisha wanaisaidia Serikali kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi chini ya Mhe. Rais wa awamu ya tano Dr. John Joseph Magufuli.
”Nimefurahi kuona viongozi wa Chama wapo hapa kushuhudia utekelezaji wa Ilani, vile vile nafarijika sana kuona darasa hili lililojengwa na OCODE na nnaahidi kuendelea kushirikiana nao” aliongeza Mkurugenzi.
”Niombe tuendelee kushirikiana kuanzia ngazi za chini hasa kwenye kukusanya mapato ili hata hawa walimu wasio na ofisi tuweze kuwajengea. Si hilo tuu lakini Manispaa yetu imefaulisha watoto wengi kwenda kidato cha kwanza hivyo bado tuna upungufu wa madarasa na huwa tunaangalia hasa pale penye uhitaji mkubwa ndio tunatilia mkazo”.Alisisitiza Beatrice.
Nae Mwalimu Mkuu wa Kibwegere Charles Kulemba alilishukuru Shirika la OCODE kwa kuwajengea darasa lakini pia alimshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic kwa kupeleka kiasi cha Shilingi Milioni 53 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa