Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo BEATRICE DOMINIC akiongozana na Wataalam wa Manispaa ya Ubungo leo amepokea makabati kutoka katika Shirika la JSI katika Kata ya Kwembe.
Wakati akikabidhi makabati hayo Mkurugenzi wa JSI kanda ya Pwani PAMELA MSEI alisema kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo tutatoa makabati 44 ambayo yatakwenda katika Kata 10 ambazo zipo katika Halmashauri ya Ubungo.
Kata hizo ni Kata ya Kwembe inakayopata makabati 8, Kata ya Goba makabati 4, Kata ya Kimara makabati 3, Kata ya Mabibo makabati 2, Kata ya Makurumla makabati 6, Kata ya Manzese makabati 2 ,Kata ya Mbezi makabati 5, Kata ya Saranga makabati 12, Kata ya Sinza kabati 1 na Kata ya Ubungo kabati 1.
Aidha Mkurugenzi wa JSI alitambulisha shirika la JSI kuwa ni shirika linalo tekeleza Mradi wa uboreshaji wa mifumo ya afya na ustawi wa jamii.Katika Wilaya ya Ubungo tutakuwa na Kata kumi ambazo kama shirika la JSI tumehakikisha tunapeleka makabati ya kuifadhia taarifa za watoto na wanawake wanaokuwa wanafanyiwa ukatili wa kijinsia na tutakabidhi fomu namba tatu piece 78 ambazo zitasaidia katika ukusanyaji wa taarifa. Aliyasema hayo Mkurugenzi wa JSI.
Baada ya kupokea Makabati hayo *Mkurugenzi Beatrice Dominic alitoa shukrani zake za pekee kwa shirika la JSI na Mkurugenzi wa JSI kwa mchango wao wa Makabati waliyoyatoa katika Kata ya Kwembe.
Nishukuru kwa JSI kwa kazi wanayofanya hasa kwa Halmashauri ya Ubungo na niagize makabati haya yakahifadhie taarifa zinazostahili kuwekwa katika makabati haya na si vinginevyo na nitafuatilia hili katika kata hizi kuliangalia hili kwa umakini na kufwatilia.
Pia niagize kwa watendaji ambao mpo chini yangu tufanye kazi kwa haki na tutekeleze yale ambayo mradi unategemea kwamba tutayafanya na sisi kama Wataalam tuhakikishe haya yanayofadhiliwa na wenzetu tunayafanyia kazi. Alisema hayo Mkurugenzi Beatrice Dominic
Aidha Nipende kusisitiza wanakamati mkiwa katika vikao vyenu mjadili mambo yote muhimu na muhakikishe mnapata taarifa sahihi za watoto wanaohishi katika mazingira magumu na muhakikishe mnashughulikia vyema na mtumie vikao mnavyofanya mtoe taarifa za sehemu mnapotoka na mziweke katika maandishi. Aliongeza Mkurugenzi Beatrice Dominic
Nae Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Ndg.PETER NSANYA alitoa shukrani zake kwa Shirika la JSI kwa mchango wao walio hutoa kwa Manispaa ya Ubungo na kuahaidi makabati hayo yatatumika ipasavyo katika kuhifadhi taarifa za watoto hao.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa