Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic amezindua mradi wa kutakasa mikono katika soko la Mabibo mradi ambao umedhaminiwa na Asasi ya kiraia ya Network for Vulnerable Rescue Foundation (NVRF) kwa kushirikiana na kundi lenye vijana 250 la Whatsapp lijulikanalo kama Vijana Think Tank(VTT)
Wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi aliambata na afisa biashara wa manispaa na maafisa masoko na Wataalam kutoka Manispaa.
Lengo likiwa ni kuzindua Mradi ulioshirikisha vijana 250 wa Vijana Think Tank (VTT)ambao walishirikiana na Foundation ya Network for Vulnerable Rescue Foundation( NVRF)
Wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi aliwashukuru kwa juhudi walizofanya na kuthamini kufanya maendeleo katika soko kwa kuona ni jambo la muhimu kuhakikisha wanasaidia wengine kujikinga na korona.
"Nasisitiza wafanyabiashara na wateja watumie maji haya na sabuni kwa kunawa mikono na si vinginevyo ili lengo la mradi litimie"alisisitiza Mkurugenzi.
Nae Mkurugenzi wa NVRF Ndg. Peter Kiangi alisema kuwa wapo kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za Serikali na ndio maana wamedhamini mradi huo wa Mabibo.
Aidha Lilian Mahenge, Makamu Mwenyekiti wa Vijana Think Tank alisema kuwa wao kama vijana waliona kuna umuhimu wa kuweka mradi huo Mabibo. Mradi huo utasaidia watu kunawa bila ya kungojeana na kusaidia shughuli mbalimbali za kiutendaji kufanyika kwa haraka.
Mwisho Mkugenzi aliwashukuru na kuwakaribisha tena Manispaa ya Ubungo ili kuendelea kuleta maendeleo kwa wana ubungo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa