Mkutano huo umefanyika tarehe 30/1/2020 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya uliopo Luguruni na kuongozwa na Meya wa Manispaa ya ubungo Mhe. BONIFACE JACOB pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo BEATRICE DOMINI Katika mkutano huo Baraza la Madiwani lilipitisha Bajeti ya mwaka 2020-2021 ambayo Manispaa ya Ubungo inategemea kukusanya/ kupokea fedha kiasi cha Tsh 104,644,876,344.86.00 kati ya fedha hizo Tsh 81,995,999,669.,86.00 ni ruzuku kutoka Serikali kuu, Tsh 20,002,948,852.00 ni fedha za makusanyo ya ndani ya Halmashauri , Tsh 1,895,927,823,.00 ni fedha za wafadhili na Tsh 750,000,000.00 ni fedha za michango ya nguvu za wananchi. Makadilio ya bajeti ya mwaka 2020-2021 imeongezeka kwa kiasi cha Tsh. 22,791,778,974.86 sawa na asilimia 27.8 ukilinganisha na makadilio ya bajeti ya mwaka unaoendelea 2019-2020.
Aidha Makisio ya matumizi kwa bajeti ya mwaka 2020-2021 Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo inatarajia kutumia Tsh 88,599,143,250.86 kwa matumizi ya kawaida ya mishahara ambayo ni sawa na asiliimia 85 ya bajeti na Tsh 16,045,816,960.00 ni fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 15 ya bajeti yote. Fedha hizo za Miradi ya maendeleo zinajumuisha kiasi cha Tsh. 8,516,769,314.00 Mapato ya ndani, Tsh 4,883,119,823.00 Ruzuku za maendeleo kutoka Serikali kuu , Tsh.1,895,927,823.00 ni fedha za wadau wa maendeleo na 750,000,000.00 ni nguvu za wananchi.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic ameshukuru kwa wageni waliokuja kwenye baraza hilo na kushukuru mapitisho ya bajeti iliyopitishwa na baraza la madiwani ya mwaka 2020/2021.
Mwisho Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo alihitimisha baraza hilo kwa kupongeza timu ya mejimenti na wajumbe wote wa kamati za kudumu wa Manispaa kwa kazi nzuri ya kuchambua makisio yote ya mapato na matumizi pamoja na miradi ya maendeleo waliyoifanya kuanzia mwanzo wa uwaandaaji wa bajeti mpaka kukamilika.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa