Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori ameongea na madereva wa bodaboda na kutoa vitendea kazi (reflector) kwa madereva ambao watakuwa ni wawakilishi katika zoezi zima la kupambana korona kwa kutoa elimu vijiweni na kwa wateja wananchi waliowazunguka kuhusiana na ugonjwa huo.
Wakati wa tukio hilo aliambatana na Katibu tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg.James Mkumbo na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dr. Peter Nsanya
Lengo kuu likiwa ni kuongea na wawakilishi wa madereva wa bodaboda kwa kata zote 14 zilizopo Wilaya ya Ubungo ambao walipewa semina kuhusu mapambano dhidi ya homa kali ya mapafu korona ili wawe wawakilishi na watoa elimu kwa jamii kuhusu ugonjwa wa korona na namna ya kujikinga.
Aidha Mkuu wa Wilaya aliwaasa madereva hao wahakikishe wanashirikiana na wananchi kwa kuwapa elimu waliyopata ya jinsi ya kupambana na korona.
Tumshukuru Rais wetu kwa hatua ambazo amezichukua kupambana korona na ni muhimu kufuata maagizo ambayo yanatolewa na Serikali pamoja na Wizara ya Afya. aliongeza Mkuu wa Wilaya.
Nasikitika kuna baadhi ya Wenyeviti ambao wanatumia nafasi zao vibaya kwa kutoa vibali vya mazishi kinyemela bila ya kufata maelekezo ya serikali juu ya sehemu ambazo zimetengwa kwa ajili ya maziko kwa ndugu zetu ambao wametangulia mbele za haki kwa magonjwa mbalimbali. Na nitumie fursa hii kuwaonya hata viongozi ambao wamekuwa wakisambaza taarifa za uongo kuhusu wahanga wa korona kinyume na utaratibu ambao Serikali imeuweka. Alifafanua Mkuu wa Wilaya
Pia Mhe. Kisare alisisitiza tahadhari ziendelee kufuatwa na watu wawe makini na kufuata maagizo yanayotolewa kwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na kuvaa barakoa.
Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo aliwashukuru madereva boda boda kwa ujio wao na kuwaomba wawe na mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya korona.
"Na niwaombe muendelee kujitoa kwa ajili ya mambo mengine pia katika kusaidia na kuleta maendeleo ya Wilaya yetu." Alisisitiza Katibu Tawala
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa