Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James akiambatana na wajumbe wa Kamati ya ULINZI na Usalama ya Wilaya hiyo ametembelea na kukagua eneo la kujenga Kituo cha Afya katika kata ya Goba kitakachojengwa na fedha za Serikali zilizotokana na Tozo za mawasiliano.
Ujenzi wa mradi huo utagharimu Jumla ya shilingi milioni 500 ambapo milioni 250 zimepokelewa Kwa awamu ya Kwanza Kwa ajili ya kuanza ujenzi huo .
Akiongea baada ya kukagua eneo hilo James amesema kuwa , Kamati imefanya ukaguzi Kwa ajili ya kuhakikisha ujenzi huo unaanza mara moja ili kufikia lengo la Serikali la kuboresha na kusogeza huduma za afya Kwa Wananchi.
Hadi sasa Manispaa tayari imepokea Tsh Milioni 250 kwa ajili ya kuanza mradi huo ambapo kwa sasa ujenzi itahisisha majengo mawili muhimu ambayo ni jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na Maabara.
Aidha, James amesisitiza wataalamu kuhakikisha ujenzi wa majengo hayo kukamilika ndani ya miezi mitatu yaani mwezi Aprili 2022.
James amesisitiza kuwa mwenye umiliki halali wa eneo hilo la mradi ni serikali pekee hivyo hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kuzuia mradi huo usifanyike na kumsisitiza OCD kuchukua hatua Kwa yeyote atakayezuia ujenzi huo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa