Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori leo ametembelea kata za Kimara na Saranga ili kujionea mwenyewe kwa macho maafa yaliyotokea kutokana na mvua kali iliyonyesha katika maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Ubungo. Mhe. Mkuu wa Wilaya aliongozana na kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Diana Nkarage.
Mhe. Makori aliwaambia wananchi wa Mtaa wa Golani Kata ya Kimara kuwa amefika kwao ili kujuliana hali na kuwapa pole wale wote walioathirika na mvua zilizonyesha tarehe 04/03 siku ya Jumatano. "Nimefika kwa niaba ya Serikali kuwapa pole wahanga wote ambao wameathirika kwa namna moja ama nyingine na mvua zilizonyesha hivi karibuni. Alisema Mkuu wa Wilaya. Mkuu wa Wilaya alisema kuwa amewasiliana na wadau ambao kama watakuwa tayari kusaidia basi Wilaya itaona namna ya kuwashika mkono.
Baada ya kutoka Mtaa wa Golani Mhe. Mkuu wa Wilaya alitembelea Shule ya Msingi Saranga iliyopo kata ya Saranga ambapo kuna madarasa matatu yaliyoezuliwa paa na nyumba mbili za walimu ambazo pia zimeezuliwa paa.
Mkuu wa Wilaya aliwahakikishia wanafunzi na walimu kuwa tayari kuna jitihada za haraka zinafanyika ili madarasa na nyumba za walimu ziweze kukarabatiwa na hatimaye wanafunzi waweze kupata sehemu ya kusomea.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa