Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori leo amefungua mafunzo (semina elekezi) kwa wenyeviti wa Serikali za mitaa na watendaji.
Mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Little Flowers uliopo Mbezi na mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori.
Wengine waliohudhuria mafunzo hayo ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Lucas Mgonja, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic, wataalam kutoka Manispaa ya Ubungo, kamati ya ulinzi ya Wilaya, viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Wenyeviti wa Mitaa na watendaji wa mitaa 90 na wa kata 14 wa Wilaya ya Ubungo.
Wakati akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya alisema mafunzo yatahusu usimamizi na uendeshaji wa shuguhuli za Mamlaka za Serikali za Mitaa.
"Ni matumaini yangu mafunzo haya yataambatana na utendaji wa kazi utakaokuwa na nidhamu, uwajibikaji ,uzalendo ambao unafanana na utendaji kazi ambao Raisi wetu wa awamu ya tano Dr. John Pombe Magufuli anauhitaji."* Alisema Mkuu wa Wilaya.
Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya aliwasisitiza wenyeviti wahakikishe wanafanya kazi kwa umakini na ukaribu na ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi ili kukamilisha majukumu kwa pamoja.
Aidha Mhe. Mkuu wa Wilaya aliwaambia wenyeviti, watendaji kuwa ni imani yake kuwa baada ya semina watafanya kazi kwa uadilifu, bidii na moyo kuhakikisha Manispaa ya Ubungo inafanikiwa.
NB Semina hiyo elekezi ni ya siku mbili na inatarajia kuisha hapo kesho siku ya ijumaa tarehe 5/3/2020.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa