Mkuu wa wilaya ya ubungo Mhe.kisare Makori atembelea wakazi waishio Mtaa wa kinzudi Kata ya Goba. Aliongozana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg. James Mkumbo, Afisa tarafa wa Kibamba Beatrice Mbawala, wataalam kutoka Dawasa na Tarura na wataalam kutoka Manispaa ya Ubungo.
Lengo la kuja katika eneo hili ni kwaajili ya kutatua mgogoro uliopo katika eneo hili la hekta 8 linalojulikana kwa jina la (shamba la mzungu), naomba niseme eneo hili tayari umiliki wake umelejeshwa mikononi mwa wananchi na sio vinginevyo. Alisema hayo Mkuu wa Wilaya
Aidha nipongeze pia kwa uongozi wa Serikali ya Mitaa kwa kuitisha kikao katika eneo hili kwani tangia nije kwa mara ya kwanza wananchi wanaokaa eneo hili walinipokea na kuonyesha ni jinsi gani walikuwa wakikerwa na aliyekuwa akisema ni mmiliki wa eneo hili na leo nimekuja kutatua changamoto hiyo inayowasumbua.
Naomba niseme kwamba eneo hili kuanzia sasa jina hilo linalotumika la ( shamba la Mzungu) lifutwe kwani tayari eneo hili ni mali ya umma na liko chini ya usimamizi wa Halmashauri yetu ya ubungoSerikali ya awamu ya tano iko vizuri na inahakikisha wananchi wake wanapata haki zao ipasavyo, chini ya uongozi wa JOHN POMBE MAGUFULI raisi wetu wa awamu ya tano naye anasimamia haki za kila mtanzania na kuhakikisha haki zinatolewa ipasavyo.
"Ilitufanye shughuli za maendeleo ni lazima kuhakikisha amani ya nchi hii tunaitunza, Pia tuhakikishe kila mmoja wetu anasimamia misingi sahihi ya utulivu na kuhakikisha analinda maendeleo ya nchi yetu"aliongezea Mkuu wa Wilaya
Pia naomba niseme kuhusu ugonjwa hatari wa corona ambao rais wetu alisema ,tujikinge na hili pia, tuchukue tahadhali ilituepukane na hili pia, tukichukua tahadhali mapema itasaidia na tutaendelea na shuguli za maendeleo katika nchi yetu. Niwakumbushe pia kuhusu swala la bima ambalo linaweza kuwa msaada kwenu nyote mkakate bima za ICHF ili kupata wepesi wakupa matibabu,na swala la mikopo pia afisa maendeleoya jamii atawapa muongozo ili vikundi mpate mikopo kwaajili ya ujasiliamali na mkawe kipaumbele kwenye kurudisha mikopo hiyo ili mnufaike zaidi,
Mwisho niwashukuru kwa ujio wenu katika eneo hili na niwahaidi kuwa nanyi katika kutatua changamoto yoyote kama Mkuu wenu wa Wilaya ya Ubungo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa