Leo Januari 19, 2023 mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amefanya ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa kituo kikubwa cha biashara (Shopping Mall) kinachotarajiwa kuanza kujengwa kesho Januari 20, 2023 katika eneo la kituo cha zamani cha Mabasi Ubungo
Mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2024, una thamani ya dola za kimarekani Milioni 118 sawasawa na pesa za kitanzania Bilioni 271 na utakua na maduka pamoja na ofisi 2,060 ambapo wafanyabiashara wadogo na wakubwa watakuwepo pamoja na watengenezaji wa bidhaa mbalimbali kutoka China hivyo wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika mashariki watapata fursa ya kuuza na kununua bidhaa zao katika kituo hiki
Mapema akiongelea mradi huo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James amesema kuwa, mradi huo unaenda kuwa na faida kubwa kwa Manispaa ya Ubungo kwa upande wa mapato, ajira kwa watanzania wengi pamoja na kuitangaza tanzania kibiashara kote Afrika Mashariki
Nae mkurugenzi wa kampuni ya East - Africa Commercial & Logistics Center ambao ndo wawekezaji katika mradi huo ndugu Catherine Wang amesema, dhamira ya mradi huo ni kuleta bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu
Akiongea katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makala amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuifungua nchi yetu kimataifa kwenye masuala ya kibiashara ambapo wawekezaji wengi kutoka nchi mbalimbali sasa wanavutiwa kuja kuwekeza Tanzania. Pia mradi huu upo katika eneo zuri kimkakati kwaajili ya biashara hivyo utaleta tija kubwa kwa nchi yetu
"Eneo hili ni zuri sana kwasababu ni makutano ya barabara zote hivyo ni rahisi kutoka sehemu yoyote ndani ya Dar es Salaam, Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Hongereni sana Manispaa ya Ubungo na Mwekezaji" Alisema Makalla
viongozi wakitazama mradi jinsi utakavyokuwa baada ya kukamilika
Aidha mradi huo unatarajiwa kuongeza mahusiano mazuri ya kibiashara na nchi mbalimbali duniani na bila kusahau mradi utaipendezesha Manispaa ya Ubungo na Dar es Salaam kwa ujumla
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa