Wananchi 450,000 wa Ubungo, Bagamoyo na maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam wanatarajia kunufaika na huduma ya maji kupitia mradi wa maji kutok Bagamoyo hadi chuo kikuu cha Ardhi ambao upo hatua za mwisho za ukamilishaji
Hayo yamebainika Leo Juni 24, 2022 wakati Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James akiambatana na timu ya wataalamu pamoja na DAWASA walipokagua mradi wa maji unaotekelezwa na DAWASA wenye thamani ya Bilioni 69
Mradi wote huo unatoka Bagamoyo - Chuo kikuu cha Ardhi DSM ambao unahusisha ujenzi wa matenki matatu ya maji (Tegeta A, Mbweni na Vikawe) pamoja na ujenzi wa vituo viwili vya kusukumia maji (Wazo na Mapinga) ambao ukikamilika unaenda kumaliza changamoto ya maji kwa maeneo mengi ikiwemo kata ya Goba na Mbezi.
Katika ziara hiyo Mheshimiwa Kheri ameridhishwa sana na utekelezaji wa mradi huo na amewaagiza DAWASA kuendelea na kasi hiyo hiyo wanayoenda nayo sasa kuelekea kwenye kukamilisha mradi huo kwa wakati.
"DAWASA mnafanya kazi nzuri sana ndani ya wilaya ya Ubungo kwenye utekelezaji wa miradi ya maji yenye nia ya kumtua ndoo mama kichwani hivyo basi kupitia miradi hii naamini tatizo la maji Ubungo litakua historia katika kipindi kifupi sana kijacho. Wananchi wanaona matenki ya maji lakini wanataka kuona maji" alisema
Nae Mkurugenzi wa miradi wa DAWASA Mhandisi Ramadhan Mtindasi, wakati akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa mradi huo, amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya pamoja na wananchi wa Ubungo kwa ujumla kuwa mpaka kufikia mwezi Disemba mwaka huu mradi huo wa maji utakua umekamilika tayari kuanza kutoa huduma kwa wananchi wakiwemo wa Wilaya ya Ubungo
#UbungoYetuFahariYetu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa