Mratibu wa CHF Manispaa ya Ubungo Leticia Meena atoa elimu ya bima ya Afya iliyoboreshwa ICHF “Improved Community Health Fund” kwa mawakala wa mabasi wa Stendi Kuu ya Mabasi ya Magufuli Mbezi lengo ikiwa ni kusaidia kuboresha afya kwa wananchi ukizingatia magonjwa ni mengi na matibabu ni gharama.
Aidha Meena ameeleza kuwa Mpaka sasa ICHF ina wanachama 31,587 ambapo ni sawa kaya 11,774 sawa na 23.4% ambapo lengo ikiwa ni kuandikisha kaya 11,774 sawa na 30% na mkakati wao ni kuhakikisha elimu inawafikia wananchi wengi zaidi kwa kufanya mikutano ya mara kwa mara kupitia maeneo yenye mikusanyiko ya watu na kutumia vyombo vya habari ili kufanikiwa kupata wanachama wengi.
Meena amesema ICHF ni bima ya Afya iliyoboreshwa ambayo inaleta uhakika wa matibabu na kwamba bima hiyo inapatikana kwa mtu mmoja mmoja kwa kulipia tsh 40,000/= au kwa familia ya watu sita tsh 150,000/= kwa mwaka mzima ambapo utapewa kadi ya mwanachama mara tu baada ya kulipia kwa kufika katika ofisi za mtendaji wa Mtaa au Kata au kwa kupiga simu kwa mratibu wa CHF kwa no 0713 21 09 55.
Aidha Meena ameelezea huduma zinazotolewa kwa wamiliki wa Bima ya CHF; Huduma za matibabu kuanzia Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya na Hospitali za Rufaa za Mikoa kokote Tanzania Bara, huduma zote za kumuona daktari, uchunguzi na dawa, huduma zote za kulazwa, upasuaji mkubwa na mdogo, huduma za afya ya kinywa na meno na huduma nyinginezo.
Aidha Afisa Ustawi wa Manispaa ya Ubungo Zainabu Masilamba amewaomba mawakala kusaidia kuzuia usafirishaji haramu wa watoto wadogo na watu wenye ulemavu kitendo ambacho ni kinyume na sheria za haki za kibinadamu na endapo wapatato taarifa hizo wawasiliane nae simu no 0714 303518 na kuwataka wakemee sana kitendo hicho kwani watoto na walemavu hao wamekuwa wakienda kutumikishwa kinyume na sheria za haki za kibinadamu.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa