Tarehe 7/8/2020 Msimamizi wa uchaguzi wa majimbo hayo Beatrice Dominic amefungua semina ya uchaguzi kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata zote 14 ambazo zipo kwenye majimbo ya Ubungo, Nane(8) kwa jimbo la Ubungo na (6) kwa jimbo Kibamba.
Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watendaji hao
Aidha msimamizi wa uchaguzi aliwapongeza kwa kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na aliwakumbusha kuwa uchaguzi ni sheria, kanuni na miongozo mbalimbali na pia aliwakumbusha kuwa swala la uchaguzi halina uzoefu.
Vilevile aliwataka kuwa makini katika zoezi lililoko mbele yao Ili kuondoa usumbufu wowote unaoweza kujitokeza.
Mwisho Aliwahakikishia kuwa ofisi yake ipo imara na wazi muda wote kwa ajili ya msaada wowote na akasisitiza kuwa wakaishi na kiapo chao muda wote wa kipindi cha uchaguzi
N.B Semina hiyo inafanyika kwa siku tatu na itamalizika Jumapili ya tarehe 9/8/2020 katika ukumbi wa Braggin uliopo Goba
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa