Mstahiki meya Manispaa ya Ubungo Jaffary Nyaigesha akutana na viongozi wa machinga( SHIUMA ) lengo ni kujitambulisha na kujadili namna ya kufikia malengo ya machinga kwa ajili ya kuboresha masilahi ya machinga
Aidha, Nyaigesha aliahidi Mambo mbalimbali ikiwemo kutembelea masoko yote kwa dhumuni la kusikiliza kero zao na kuongea na viongozi wake
Nae, Kiongozi wa machinga kutoka mkoani Hamis hamis ameshukuru
kwa mapokezi mazuri na kutujali
Aliendelea kwa kusema kuwa, Kama uongozi tunashughuli tunazifanya ikiwemo kutengeneza kanzi data kwa kushirikiana na Halmashauri na kuwasilisha wizarani
Ndio maana tumepita kuwatambulisha viongozi halali wa machinga kwa mkoa wa Dar na Wilaya ambao wanatambulika na shirikisho na hati ya utambulisho
Sambamba na hayo M/kiti wa shirikisho la machinga ubungo Immanuel Donas tunamefurahi kukutana na uongozi tunaendelea kuahidi kutoa ushirikiano na hata changamoto zozote tutaziwasilisha ili ziweze kupatiwa ufumbuzi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa