Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Mheshimiwa Jaffary Juma Nyaigesha amewasitiza wajumbe wa baraza na wataalam kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kupitia vyanzo mbalimbali
Mstahiki Meya ametoa kauli hiyo baada ya Halmashauri kukusanya shilingi bilioni 5.17 sawa na asilimia 18 badala ya asilimia 25 iliyopaswa kukusanywa katika kipindi Cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022
" Kazi ya ukusanyaji wa mapato ni yetu sote hivyo ni lazima tushikamane na kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha tunasimami ukusanyaji wa vyanzo vilivyopo na kubuni vyanzo vipya" alieleza Jaffary
Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Manispaa ya Ubungo imekasimia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 27 ikiwa ni mapato ya ndani kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato fedha ambayo itatumika kwaajili ya matumizi ya utekelezaji wa miradi na shughuli nyingine za maendeleo
Aidha mstahiki Meya ametumia baraza ilo kuwaeleza wajumbe kuwa Halmashauri ya manispaa ya Ubungo imepata tuzo ya kuwa Halmashauri Bora Tanzania katika matumizi ya TEHAMA iliyotolewa tarehe 22, oktoba,2021 jijini Arusha kwenye Mkutano Mkuu wa TEHAMA wa mwaka
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa