- Leo Oktoba 22, 2022 Diwani wa kata ya Msigani Mhe. Siraju Mwasha amezindua mashindano ya mchezo wa soka yanayofahamika kama MWASHA SUPER CUP katika uwanja wa Zoni uliopo Msigani
- Akizungumza katika Uzinduzi huo Mhe. Mwasha amesema michezo ina faida nyingi katika jamii ikiwemo kujenga afya, kuleta ushirikiano, kupunguza vitendo vya uhalifu pamoja na kutengeneza ajira hivyo basi amewasihi wanamichezo wote wanaoshiriki ligi hiyo kuonesha ubora wao wote kwani ligi hiyo inafuatiliwa na watu wengi kutoka maeneo mbalimbali wenye weledi tofauti tofauti katika mpira wa miguu
- Ligi hiyo itashirikisha timu 10 kutoka mitaa mbalimbali ya kata ya Msigani ambapo itadumu kwa muda wa mwezi mmoja. Mechi ya ufunguzi leo ilikua ni kati ya Malamba Combined dhidi ya Msigani ambapo matokeo ni Msigani imeshinda goli moja kwa bila
- Aidha mshindi wa kwanza katika ligi hiyo atajinyakulia kitita cha shilingi laki tano pamoja na kwenda kucheza mkoani na timu mojawapo kati ya timu zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara, Mshindi wa pili atapata shilingi laki tatu na mshindi wa tatu atapata shilingi laki mbili
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa