Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi (MB) amesema Serikali ya awamu ya sita ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya miezi 20 ya uongozi wake imeendelea kusimamia stahiki za watumishi ikiwemo upandaji wa madaraja, kulipwa kwa malimbikizo ya mishahara na mengine mengi mazuri ya kiutumishi.
Hayo ameyasema leo akiwa kwenye ziara yake ya kuitembelea Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wakati anasikiliza changamoto za watumishi wa manispaa hiyo ambapo pia alifanya ukaguzi wa kikundi cha wanufaika wa TASAF wilayani humo.
Ndejembi amewataka watumishi wa Manispaa hiyo kuhakikisha wanampango kazi wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku ikiwa ni pamoja na kuwa wabunifu, kuwajibika ipaswavyo na kutoa huduma bora ili kuendelea kutatua kero za wananchi kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.
Watumishi wa Manispaa ya Ubungo wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi (MB) (hayupo pichani) alipotembelea halmashauri hiyo.
Aidha, Ndejembi amewataka watumishi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg. Beatrice Dominic ameeleza kuwa Manispaa ya Ubungo ina idadi ya watumishi 4,397, watumishi 218 walibadilishiwa Muundo kutokana na kujiendeleza kielimu, 742 wamepanda madaraja kwa mujibu wa kanuni za kiutumishi na watumishi 1,559 malimbikizo yao yalilipwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi (MB) akikagua kikundi cha wajasiliamali kinachonufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) Ubungo
Nae Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Kheri James amesema Manispaa ya Ubungo inajivunia kwa mapinduzi makubwa yanayofanywa na Serikali katika kuleta mageuzi ya haki na kuzingatia stahiki za watumishi.
“Tunaona mageuzi makubwa yanayofanywa kwenye upandishwaji wa vyeo kwa watumishi, mafao ya watumishi, ongezeko la mishahara ya watumishi na mengine mengi mazuri yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita” Alisema James.
@utumishi8
@dndejembi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa