Watumishi Manispaa ya Ubungo wamemshukuru Mhe. Rais wa Jamuhuli wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa utendaji kazi wake ikiwemo kuboresha maslahi ya watumishi wa umma kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu aingie madarakani.
Akiongea kwa niaba ya Watumishi wa Manispaa hiyo Naomi Masangopole mbele ya waandishi wa habari leo agosti 5, 2022 na kueleza mafanikio ambayo Rais ameyafanya kwa kipindi Cha mwaka mmoja ikiwa ni pamoja na ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma, punguzo la madeni kwa upande wa mikopo ya Elimu ya juu ambayo watumishi wengi walikua wanadaiwa,
Watumishi wameendelea kumshukuru Rais kwa kupandisha madaraja watumishi ambapo kwa Manispaa ya Ubungo jumla ya watumishi 2199 wamepandishwa madaraja ndani ya mwaka mmoja na kuleta watumishi wa ajira mpya 68 kwa kada mbalimbali.
Pia, wamempongeza Rais kwa ongezeko la mishahara la 23.3 ambalo imelenga kuwainua wenye viwango vya chini Cha mshahara na kueleza kuwa jambo hilo ni kubwa kwani linaendelea kutengeneza usawa baina yetu na kuongeza ari ya kufanya kazi
"Sisi kama watumishi tunamuahidi mheshimiwa Rais kuendelea kuchapa kazi kwani tunamuelewa dhamira yake" waliahidi watumishi hao.
Aidha, watumishi hao wamewapongeza viongozi wa Wilaya hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kwa uongozi wao makini katika kumsaidia mheshimwa Rais kutekeleleza mjukumu yake ya kuhudumia wanannchi hususani usimamizi wa miradi na ukusanyaji wa mapato.
Pia watumishi hao wametumia nafasi hiyo kuwakumbusha watumishi wa umma, viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla kushiriki katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika tarehe 23.8.2022 kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo ya Taifa letu.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa