Mkuu wa Mkoa wa dar es salaam, Mhe.Aboubakar Kunenge ameipongeza Halmashauri ya manispaa ya ubungo Kwa kufanikiwa kutoa fidia ya shilingi milioni 991 na kupata eneo la ujenzi wa soko la wajasiliamali wadogo la mbezi Luis ambapo ujenzi huo upo hatua za umaliziaji.
Pongezi hizo amezitoa leo wakati alipotembelea na kukaugua utekelezaji wa mradi huo na kueleza kuwa ujenzi wa soko hilo ni agizo la serikali la kutenga maeneo maalumu Kwa ajili ya wajasiriamali wadogo kote nchini.
Kunenge ameeleza kuwa "Kwa Mkoa wa Dar es salaam changamoto kubwa ilikuwa kupata maeneo maalumu ya kuwaweka wajasiliamali wadogo nawapongeza Manspaa ya ubungo Kwa kuweza kupata eneo hili"
Aidha Kunenge amewahakikishia wajasiliamali wadogo wa eneo la mbezi uwepo wa wateja kwani eneo linapojengwa soko ni karibu kabisa na stendi mpya ya Mbezi hivyo wateja watakuwa wa uhakika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic amesema soko hilo limepanga kujenga mabanda 7 ambapo 5 yamekamilika
Baada ya kukamilisha mradi jumla ya wajasiliamali 644 watanufaika na ujenzi wa soko hilo ambapo kila Banda litachukua wajasiliamali 92.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa