Mkuu wa mkoa wa Dar Es salaam, Abubakar Kunenge leo januari 22, 2021amekabidhiwa msaada wa madawati 400 kutoka benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono agizo la mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli la kutaka wanafunzi wasikae chini ikiwemo wanafunzi wa shule ya msingi king'ongo.
Benki ya NMB imekabidhi madawati hayo katika shule ya msingi king'ongo ambapo kunajengwa madarasa tisa (9) kufuatia agizo la Mhe Rais la kutaka wanafunzi wa shule hiyo wasikae chini Wala kusomea nje.
Akiongea kabla ya kukabidhi madawati hayo , Kaimu Mkuu wa Fedha wa benki hiyo ndugu Benedicto Baragomwa amesema kuwa madawati 150 kati ya 400 yaliyotolewa na benki hiyo ni kwa ajili ya shule ya msingi King'ongo huku yanayobaki kupelekwa shule ya Makabe, Kibwegere, Mpigimagoe na shule ya sekondari Kimara kwa lengo kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati katika shule hizo.
Baragomwa ameeleza kuwa "Tulipoona changamoto ya ukosefu wa madawati katika shule ya msingi King'ongo sisi kama taasisi ya Nmb tukaona tutoe msaada wa madawati haya katika kuendeleza juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifunzia kwa kujenga madarasa na kutengeneza madawati ili wanafunzi wasome kwenye mazingira magumu
Mkuu wa mkoa wa Dar Es salaam Mhe Abubakar Kunenge ameishukuru benki ya Nmb kwa msaada wao kwani utasaidia kupunguza changamoto ya madawati kwenye shule za Mkoa you hasa shule ya King'ongo ambayo baadhi ya wanafunzi walikuwa wanakaa chini.
Kunenge amewaeleza wananchi kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau inaendelea kutatua kero zao mbalimbali ikiwemo kujenga miundombinu ya madarasa pamoja kutegeneza madawati ambapo kwa sasa jumla ya madawati elfu arobaini (40,000) yapo katika hatua mbalimbali za utengenezaji ili kumaliza kabisa changamoto ya madawati katika shule za Mkoa huo.
Kwa upande wa madarasa, Kunenge amesema Mkoa una upungufu wa madarasa 339 na kazi ya ujenzi wa madarasa hayo inaendelea na yanatarajia kukamilika februari 28 2021 ambapo mpaka leo jumla ya madarasa 97 yameshakakilika
"Niwahakikishie wananchi wa king'ongo na Dar Es salaam kwa ujumla kuwa tumejipanga kutatua changamoto za madarasa na madawati katika shule zote ili wanafunzi wawe na mazingira bora ya kujifunza na kujifunzia"
Kunenge ameengpdelea kueleza kuwa, matokeo ya mitihani wa darasa la saba mwaka 2020 , mkoa wa Dar Es salaam uliongoza kutokana na juhudi za serikali na ufundishaji mzuri wa walimu, hali iliyopelekea uwepo wa wanafunzi wengi katika shule za sekondari. Aidha kwa upande wa shule za misingi hadi kufika mwezi machi mwaka huu, jumla ya wanafunzi wa darasa la kwanza elfu sabini na nane (78,000) yanatarajiwa wameandikishwa.
wanafunzi, ameishukuru benki ya NMB kwa msaada wa madawati hayo kwani wanafunzi sasa waliokuwa wanakaa chini watakuwa wanakaa kwenye madawati hali itakayosakdia wanafunzi kujifunza katika mazinga mazuri.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa