Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam, Abubakar Kunenge leo januari 21, 2021 amepokea msaada wa mifuko 800 ya saruji kutoka kiwanda cha Saruji cha Twiga jijini Dar Es salaam kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya madarasa ya shule za msingi na sekondari za Manispaa ya Ubungo.
Mara baada ya kukabidhiwa msaada huo katika eneo la kiwanda hicho, Kunenge amemkabidhi mifuko hiyo ya saruji Mkuu wa Wilaya y Ubungo mhe. Kisare Makori kwa ajili ya kukarabati madarasa chakavu na ujenzi mpya wa madarasa katika shule za Manispaa ya Ubungo ikiwemo shule ya msingi King'ongo inayoendelea na ujenzi wa madarasa 9 kwa sasa.
Rc Kunenge akikagua mradi wa ujenzi wa madaraka 9 shule ya msingi king'ongo
Kunenge amekishukuru kiwanda cha saruji cha Wazo hill kwa msaada huo hasa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka ambacho shule zinapokea wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza hivyo uhitaji wa miundombinu ya madarasa ni mkubwa sana.
Kwa mwaka huu 2021,Kunenge ameeleza kuwa kutokana na mafanikio ya sera ya elimu bila malipo Mkoa wa Dar Es salaam umeandikisha jumla ya wanafunzi elfu 78 kwa ajili ya kujiunga na darasa la kwanza.
Kutokana na idadi ya uandikishwaji huo kuwa mkubwa umepelekea Mkoa kuwa na upungufu wa madarasa 337 kwa shule za sekondari ambapo madarasa hayo yameanza kujengwa na yapo katika hatua mbalimbali na yanatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi februari.
Kunenge amesema kuwa "Nina amini, kwa Wilaya ya Ubungo mifuko hii ya saruji niliyowakabidhi itakwenda kutatua kabisa changamoto ya madarasa kwa shule za msingi na sekondari, kaitumieni vizuri"
Maendeleo ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi king'ongo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa