Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameagiza Mabasi yote yaendayo mikoani na nchi jirani kuhakikisha yanapakia na kushusha abiria kwenye kituo kikuu Cha Mabasi Cha Mabasi cha Magufuli na sio sehemu nyingine yoyote.
Agizo hilo amelitoa leo julai 9, 2021 wakati alipotembelea kituo hicho na kusikiliza kero mbalimbali za Wafanyabiashara kituoni hapo na kueleza kuwa kituo kikuu cha mabasi ni kimoja cha Magufuli kilichopo Mbezi.
Makalla amesema kuwa, Serikali imewekeza fedha nyingi kujenga kituo hicho na ndio kituo pekee cha Mabasi hivyo hakutakuwa na maana kama kila mmiliki wa mabasi atakuwa na kituo chake cha kupakia na kushusha abiria.
"Kutoshusha na kupakia abiria kwenye kituo hiki kikuu cha mabasi kunaipotezea Serikali mapato jambo ambalo ni mhimu katika kuendelendeza kituo na miradi mingine ya maendeleo" alifafanua Makalla.
Katika kuhakikisha agizo hilo kinatekelezwa, Makalla amelielekeza jeshi la polisi kuhakikisha mabasi yote yanashusha na kupakia abiria kwenye kituo hicho na si vinginevyo,
Makalla ameelekeza uongozi wa Stendi hiyo kuweka utaratibu wa baadhi ya Mabasi kushusha abiria kwenye eneo la kulaza magari ambapo kuna Banda la Mamalishe na babalishe ili kuchangamusha biashara.
Kuhusu soko la wajasiriamali lililopo karibu na Kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli, RC Makalla ameelekeza Wafanyabiashara wote wahamishiwe sokoni hapo kwani Wafanyabiashara hao wamesema wapo tayari kuhamia sokoni hapo baada ya changamoto zilizopo kutatuliwa.
Ili kuhakikisha wajasiriamali wa soko Hilo wanapata Wateja , Makalla ameagiza uwekwe utaratibu wa kushusha abiria sokoni hapo ikiwa ni njia ya kusogeza Wateja.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa