- Ni baada ya Mtendaji wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi ndugu Kelvin Mowo kushambuliwa na kuuawa ofisini kwake Jana october 11,2021
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam Amos Makalla ameagiza Ofisi zote za Kata na Mitaa kuwa na walinzi ili kuepusha vitendo vya uhalifu ikiwemo kuvamia na kuwadhuru watumishi Wakati wakitekeleza majukumu yao.
Makalla amesema hayo kufuatia kifo cha Mtendaji wa Mtaa wa msumi kata ya Mbezi ndugu Kelvin Mowo baada ya kishambuliwa Kwa mapanga na watu wasiojulikana Jana october 11,2021 ofisini kwake akiwa anaendelea kutekeleza majukumu yake ya kutatua mgogoro wa ardhi.
Makalla amesema "Ninaagiza kuanzia sasa Ofisi zote za Mitaa na kata kuwa na polisi Jamii au mgambo waliopitia mafunzo Kwa ajili ya kusimamia ulinzi na usalama katika Ofisi hizo sambamba na kufanya ukaguzi kwa kila anayeingia ofisini kupata huduma"
Aidha, Makalla amewasihi wananchi kuacha tabia ya kuchukua sheria mkononi ya kuwadhuru watumishi au wananchi wenzao na kueleza kuwa vyombo vya Sheria ndivyo vyenye mamlaka ya kutoa haki Kwa kujibu wa sheria na sio vinginevyo
Nae kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar Es salaam ndugu Jumanne Muliro Jumanne alisema kuwa mpaka sasa watuhumiwa watatu wanaodaiwa kufanya kitendo hiko Jana Oktoba 11, katika ofisi ya Afisa Mtendaji huyo wakati alipokuwa anatekeleza majukumu yake ya kusikiliza mgogoro wa ardhi wamekamatwa na upelelezi unaendelea.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa