- Katika kuendeleza jitahidi za kuibua vyanzo vipya vya mapato ya ndani ya Halmashauri, Mapema leo Novemba 15 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amezindua rasmi mradi wa Hotel ya "Ubungo Executive Lodge" iliyopo katika kituo kikuu cha Mabasi cha Magufuli.
Akizindua hotel hiyo, RC Makalla ameelekeza hotel kuachwa ijiendeshe kibiashara ili kuleta tija kwa serikali na mwekezaji pia.
Aidha RC Makalla ametaka uendeshaji wa hotel hiyo kuzingatia makubaliano ya kimkataba na uwazi katika kila kitu.
Hoteli hiyo Ina idadi ya vyumba 38 ambavyo vikijaa vyote itaingiza Shilingi Milioni 1.1 kwa siku, Milioni 30 kwa mwezi na Milioni 421 kwa Mwaka ambapo Halmashauri ya Ubungo itachukuwa Asilimia 60 na Mwekezaji Asilimia 40.
Pamoja na hayo RC Makalla ametumia Uzinduzi huo kukemea Wizi na uharibifu wa Vifaa kwenye hotel huku akielekeza Halmashauri ya Ubungo kutafuta Wadau watakaoboresha mandhari ya nje ya Kituo Cha Magufuli ikiwemo Ujenzi wa bustani na sehemu za kupumzika kulingana na hadhi ya Kituo.
@ortamisemi
@daressalaam_rs_digital
@ubungo_executive_lodge
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa