Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Amos Makalla ameipongeza Wilaya ya Ubungo kwa kuwa wa kwanza kukamilisha Ujenzi wa madarasa 151 kwa shule 21 ikiwa ni maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato Cha kwanza kwa Mwaka 2022 na kuingia rasmi tarehe 17.1.2022 katika madarasa hayo yakiwa yamekamilika
Makalla ameyasema hayo Leo tarehe 5.1.2022 alipotembelea Ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Makabe iliyopo Kata ya Mbezi yenye madarasa 20 yaliyokamilika na ni shule mpya inayoenda kupokea wanafunzi kwa awamu ya kwanza waliofaulu kujiunga na kidato Cha kwanza Mwaka 2022
Aidha Makalla amemshukuru Mheshimiwa rais wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kwa mgao wa fedha za mpango wa Taifa kwaajili ya Mapambano Dhidi ya Uviko-19 ambazo zimeenda kuboresha sekta ya elimu na kupunguza changamoto ya uchache wa madarasa kwa wananfunzi wanaojiunga kidato Cha kwanza
Makalla amewapongea viongozi akiwemo mkuu wa Wilaya , Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo na mstahiki meya kwa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo kwa uweledi
Nae Mwenyekiti wa chama mkoa Kate Kamba amewahasa wananchi kujitokeza kwa wingi kuchanja chanjo ya Uviko-19 ilikujikinga na ugonjwa huo
Napia ametoa pongezi zake kwa Uongozi wa Wilaya ya Ubungo kwa kuonyesha umahili na uweledi kwa kusimamia mradi kuwa wenye ubora na viwango
Alikadhalika Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kheri James amemshukuru Makalla kwa ujio wake na pongezi alizotoa na kuahidi kuendelea kusimamia na kutekeleza majukumu yote kwa ufasaha
Sambamba na hayo mwananchi wa eneo hilo ambaye pia ni mjumbe Bi. Mwantumu Ramadhani amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kwaajili ya fedha zilizotolewa kwaajili ya Ujenzi wa madarasa kwani shule hiyo inaenda kuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Makabe na kata ya mbezi kwa ujumla
Ujenzi wa madarasa hayo yametokana na fedha za mgao wa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya Uviko-19 ambapo katika mgao huo Manispaa ya Ubungo ilipokea bilioni 3.02 kwaajili ya Ujenzi wa madarasa 151 kwa shule 21
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa