Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makalla ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwajuhudi za ukamilishaji wa mradi wa ujenzi wavyumba madarasa 81 ikiwa ni maandalizi yakuwapokea wanafunzi 15,008 wakiwemowasichana 7,632 na wavulana 7,376 wa kidatocha kwanza kwa mwaka 2023.
Amezitoa Pongezi hizo wakati wa ziara ya kikaziya kukagua utekelezaji wa mradi wa madarasakatika Manispaa hiyo lengo ikiwa ni kuhakikishamiradi hiyo inatekelezeka kwa ufanisi nakukamilika kwa wakati ambapo ameridhishwa nakasi na kiwango cha ubora katika utekelezaji wamradi huo
Makalla alieleza kuwa, Mkoa wa Dar es Salaam umepokea shilingi Bilioni 12.3 kwa ajili ya ujenziwa vyumba vya madarasa 618 mkoani humoambapo Manispaa ya Ubungo ilipokea shilingiBilioni 1.62 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 81 vyamadarasa kwenye shule 10 za Sekondari zaManispaa hiyo.
“Hakika bila kupepesa macho Ubungo mmefanyavizuri kwenye utekelezaji wa mradi huu, na nidhahili madarasa haya yatakamilika kwa wakatikama mlivyofanya kwenye madarasa ya Uviko” Alisema Mhe. Makalla.
Pamoja na pongezi hizo , Makalla amemtakaBeatriceDominic Mkurugenzi wa ManispaaUbungo kuhakikisha maeneo yote ya shuleyanapimwa na kuwa na hati miliki ya ardhi pamojana kuwekewa uzio ili kukabailiana na changamotoya uvamizi wa maeneo hayo. Aidha wananchiwametakiwa kulinda miundombinu yote ya shuleili shule hizo zibaki katika ubora wake nakutumika kwa muda mrefu.
“Wananchi na Wenyeviti wa Mitaa lindeni mipakaya Shule zilizopo kwenye maeneo yenu ilikuepuka uvamizi wa maeneo ya Shule hizo” alisisitiza Makalla.
Kwa upande wake Beatrice Dominic Mkurugenziwa Manispaa hiyo amesema katika utekelezaji wamradi wa madarasa hayo madarasa 27 yameshakamilika na madarasa 54 yako kwenyehatua ya ukamirishaji ambapo hadi kufikia tarehe25 Disemba, 2022 madarasa yote yatakuwayamekamirika yakiwa na viti na meza zawanafunzi.
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ilipokeakiasi cha shilingi Bilioni 2.62 kwa ajili ya ujenzi wavyumba vya madarasa 81 katika shule 10 zilizokuwa na upungufu wa madarasa kwa ajili yakupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwamwaka wa masomo 2023.
Kwa mwaka 2023 Manispaa ya Ubungo inatarajiakupokea idadi ya wanafunzi 15,008 wakiwemowasichana 7,632 na wavulana 7,376 wa kidatocha kwanza ambao watakuwa na uhakika wakusoma wakiwa madarasani kwani Rais waawamu ya sita Mheshimiwa Dkt. Samia SuluhuHassan ameendelea kuboresha vya kutoshamiundombinu ya elimu kwa maslahi ya wananchiwa Tanzania.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa