- Awataka LATRA kutokwepa majukumu Na nyaraka zao walizotoa kwa stendi binafsi
- Aruhusu stendi binafsi 5 zilizohakikiwa Na LATRA kuendelea kutoa huduma Kwa sharti la kuingia na kutoka wapitie stendi Magufuli
- Aagiza Manispaa ya Ubungo kukaa Na wamiliki wa stendi binafsi kuona njia bora kukusanya mapato
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametangaza kuondoa katazo lililokuwa likizuia Mabasi yaendayo mikoani na nje ya Nchi kutoruhusiwa kupakia abiria au kushusha katika Vituo binafsi na badala yake ameruhusu utaratibu huo kuendelea Kwa sharti la kila basi kuingia ndani ya Kituo kikuu Cha Mabasi Cha Magufuli
RC Makalla ametoa maamuzi hayo wakati wa kikao Cha pamoja baina ya LATRA, Wamiliki wa Stendi binafsi na Halmashauri ya Ubungo na kubaini pasipokuwa na shaka kuwa Waliotengeneza Vituo binafsi walifuata taratibu na kupatiwa Vibali na LATRA Baada ya kukidhi vigezo
Miongoni mwa vigezo vilivyotolewa na LATRA ili kuruhusiwa kuanzisha Stendi binafsi ni pamoja na uwepo wa Vyoo, Sehemu ya mapumziko kwa abiria, viburudisho Na sehemu ya maegesho
Kutokana na Hilo RC Makalla ameridhia Vituo binafsi 5 vilivyohakikiwa kuendelea kutoa huduma na kufungua milango kwa wamiliki wengine wanaohitaji kuwa na Vituo binafsi kushirikiana na LATRA ili wapatiwe vigezo vinavyohitajika ambapo wamepewa Mamlaka ya kufuta au kutoa leseni
Aidha RC Makalla ameagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kukaa kikao Mara moja na wamiliki wa Stendi binafsi ili kuona njia Bora ya ukusanyaji wa mapato
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa