Leo Agosti 11,2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam AMOS MAKALLA ametembelea Stendi ya Mabasi Magufuli na kutatua changamoto zinazoikumba stendi hiyo na kutoa maagizo kwaajili kuimarisha utoaji wa huduma katika stendi hiyo
CHANGAMOTO 5
- Baadhi ya mabasi kushusha na kupakia abiria nje ya kituo
- Uwepo wa ofisi ya kutolea huduma nje ya kituo(Vituo bubu)
- Askari wa SUMA JKT kwa kushirikiana na watoza ushuru kuruhusu abiria kupita getini bila ya ticket
- uharibifu wa miundombinu kutokana na uwepo wa watu wasio kuwa na sifa katika kituo
-uwepo kwa wafanyabiashara pembezoni mwa kituo
MAAGIZO
-Wale wote wanaoingia stendi bila ya kuwa na risiti baada ya wiki tatu utaratibu mpya utaenda kutumika
-Mkuu wa Wilaya , uongozi wa Manispaa iweze kuelekeza watu rasmi wanaotakiwa kuwepo stendi wajulikane ilikuepusha uharifu wa miundombinu na kuepusha wizi katika stendi
-Tanroad , Jeshi la polisi tufanye kazi kwa kusimamia usalama wa kituo na watu waliokuwepo stendi
-LATRA ishughulikie swala la Vituo bubu
*Nataka kusisitiza katika Mambo yafuatayo*
MAELEKEZO
•Swala la ulinzi na usalama lizingatiwe katika kituo
•Mkurugenzi wa LATRA , Mkuu wa Wilaya , wamiliki wa Vituo, wakae na wamiliki wote wa mabasi wanaoshusha na wasioshusha watoe mrejesho wa Mapendekezo kwa muda wa siku 14
•Magari yote yapite ndani ya stendi ya mabasi ya magufuli
- Na swala la kufanya biashara masaa 24 nafanyia tathimini katika maeneo yatakayofanya biashara hizo kwaajili ya kuimarisha swala la usalama
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa