Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amesema Serikali imetoa kiasi Cha Shilingi bilioni 5.4 kwaajili ya Ujenzi wa Tank kubwa la kuhifadhi Maji la ujazo wa Lita Milioni sita ambalo Ujenzi wake unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia Sasa na kukamilika Mwezi Juni mwakani.
RC Makalla amesema ujenzi wa tanki hilo utasaidia usamabazaji wa maji Safi na Salama kwa Wakazi wa Jimbo la Kibamba na maeneo jirani ikiwemo Kwembe, Machimbo, Kibwegere, Msigani, Msakuzi kaskazini, Msumi na Kibamba mji mpya.
Aidha, RC Makalla amesema Ujenzi huo unaenda sambamba na miradi ya *Ujenzi wa visima ambapo amewaelekeza DAWASA kusimamia Mradi huo ukamilike mapema na kuleta tija kwa Wananchi.
Hayo yote yamejiri wakati wa Mwendelezo wa ziara ya yake ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi ambapo kwa jana agosti 31 ilikuwa ni zamu ya wananchi wa Jimbo la Kibamba.
Katika zoezi hilo, RC Makalla amefanikiwa kusikiliza na kutatua jumla ya kero 96 zilizowasilishwa na wananchi wa jimbo hilo na kupatiwa majibu ya papo kwa papo na zile zilizoonekana kuhitaji ufuatiliaji wa kina amezikabidhi kwa idara husika kwa ajili ya utatuzi kwa mujibu wa Sheria.
Miongoni mwa kero zilizoonekana kushamiri ni Migogoro ya ardhi Kata ya Kwembe ambapo RC Makalla amemwelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Vyombo vya dola na idara ya Ardhi kufanyia kazi Jambo hilo kwa kuanza kudhibiti tatizo mapema kabla halijawa kubwa.
Aidha, RC Makalla amewapongeza wananchi wa jimbo la Kibamba kwa kujitokeza kwa wingi kutoa kero zao ambazo kwa kiasi kiasi kikubwa zimefanyiwa kazi, ametumia nafasoi hiyo kuwaeleza viongozi na watendaji kuendelea kuwa na utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi kwa ni serikali ya awamu ya sita inataka kero za wananchi zitatuliwe kwa wakati kabla wananchi hawajalalamika ngazi zingine.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa