Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Mhe.Paul Makonda amemaliza ziara yake wilayani Ubungo na kukabidhi miradi ya maendeleo iliyotekelezwa Wilaya ya Ubungo tangu Mhe. Rais wa awamu ya tano Dr. John Pombe Magufuli aingie madarakani kwa Viongozi wa Chama Mkoa.
Katika ziara hiyo aliongozana na Kamati ya siasa Mkoa ikiongozwa na Mwenyekiti wa chama cha CCM Mkoa Bi. Katte Kamba, Katibu wa chama Mkoa Ndg. Zakaria Mwansasu, na kupokelewa na Viongozi wa chama Wilaya wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama Wilaya ya Ubungo Ndg. Lucas Mgonja Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori Mkurugenzi wa Manispaa Beatrice Dominic na wataalam kutoka Manispaa hiyo.
Miradi iliyotembelewa na kukabidhiwa ni Mradi wa ujenzi wa barabara ya Shekilango na viunga vyake 4 ya urefu wa KM 7.5, Mradi wa ujenzi ya Wodi ya wagonjwa na chumba cha upasuaji kituo cha Afya Sinza, Upanuzi wa mto Ng'ombe KM8.5 na mto Kiboko KM 3.5, Kuona kazi za wajasiriamali Vikundi 20 waliopewa mikopo na Halmashauri jimbo la Ubungo eneo la SIMU 2000 Mawasiliano, Ujenzi wa daraja la juu la Ubungo (Ubungo Flyover).
Miradi yote iliyotembelewa kwa jimbo la Ubungo ilikuwa na gharama ya Tsh Bilioni 359,208,475,450.71 na kwa jimbo la Kibamba ilikuwa na gharama ya Tsh.Bilioni 200,471,501,998.70 na jumla ya miradi hiyo kwa Kibamba na Ubungo ilikuwa na gharama ya Tsh 559,679,977,449.41
”Nitoe pongezi kwa viongozi wa Wilaya ya Ubungo kwa ujenzi unaoendelea katika kituo cha Afya cha Sinza Palestina chenye uwezo wa kutibu wagonjwa wengi kwa juhudi wanazoendelea nazo za upanuzi wa jengo hilo” alisema Mkuu wa Mkoa.
Alisisitiza kuwa waliopata mikopo ilikuwa ni agizo la Mhe. Rais na ilikuwa ni sera ya Chama cha Mapinduzi katika kuhakikisha wajasiriamali wadogo wananufaika na mikopo hiyo.
”Kuanzia leo tarehe 1/7 shughuli zote ziendelee wananchi waendelee kufanya shughuli zao waweze kupata kipato na wasiwe na hofu na pia boda boda na bajaji zote kutoka mahali popote zifanye kazi zake bila kusumbuliwa na ziingie mjini kama kawaida ila kwa kufuata sheria na taratibu” aliongeza Makonda.
Mwisho Mwenyekiti wa chama Mkoa aliipongeza Wilaya ya Ubungo kwa miradi mikubwa na yenye viwango vya juu na kusisitiza kuendelea kuwahudumia wananchi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa