Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametembelea Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo zilizopo Luguruni kata ya Kwembe ili kujionea ujenzi unavyoendelea.
Wakati wa ziara yake hiyo aliongozana na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic na Wataalam kutoka Manispaa ya Ubungo.
Aidha Rc alitoa agizo la ujenzi wa jengo la Halmashauri kuhakikisha unamalizika kabla ya Julai 31 ikiwa ni miezi miwili kuanzia sasa na ofisi hizo zianze kutumika.
Sambamba na hilo aliwataka kuhakikisha wanafanya kazi kwa mda rasmi uliopangwa na kumaliza miradi yote kabla ya Agosti 31 ikiwa ni moja ya kuhakikisha ahadi za serikali zinakamilika kwa wakati kulingana na Ilani ya Chama na sio vinginevyo.
"Nimetoa angalizo kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote kuhakikisha miradi inakamilika kabla ya Agosti 31"alisisitiza RC
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa