Hayo yamejiri wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kupokea na kukabidhi miradi ya Maendeleo kwa uongozi wa chama mkoa inayotekelezwa katika Manispaa ya Ubungo hususani jimbo la Kibamba.
Katika ziara hiyo RC aliongozana na Kamati ya Siasa ya Mkoa ikiongozwa na Katibu wa chama Mkoa Ndg. Zakaria Mwansansu na kupokelewa na Viongozi wa Chama Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg.James Mkumbo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Wataalam kutoka Manispaa ya Ubungo.
"Tusipimane uwezo" Hiyo ilikuwa kauli ya Mhe. Paul Makonda kwa TBA wakati wa ukaguzi wa mradi wa Ofisi za Manispaa ya Ubungo.
Baada ya ukaguzi huo Mhe. Mkuu wa Mkoa aligoma kukabidhi mradi huo kwa Chama cha Mapinduzi na kuwapa TBA muda wa mwezi mmoja hadi tarehe 30 July mradi huo uwe umekamilika kwa ajili ya kukabidhiwa.
Sambamba na hiloMiradi iliyotembelewa ni kuona kazi za Wajasiriamali vikundi 20 waliopewa mikopo na Halmashauri na katika mradi huo Mkuu wa Mkoa alikabidhi bajaji 22 kwa vikundi vilivyokidhi vigezo, Mradi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro(Kimara-Kibaha)njia nane ikihusisha ujenzi wa daraja la Kibamba, Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Manispaa ya Ubungo uliopo Luguruni, Mradi wa Ujenzi wa Stendi ya Mabasi Mbezi Luis na Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kimara
Lengo la ziara hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kukabidhi miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa Ilani ya CCM na ahadi za Mhe. Rais kwa kipindi cha miaka mitano ya Mhe. Dr. John Pombe Magufuli kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
"Niendelee kutoa shukrani za pekee kwa Mhe. Rais wa awamu ya tano kwa maendeleo anayoendelea kuyaleta kwa wananchi wa Wilaya ya Ubungo na kwa kauli yake kuwa maendeleo hayana chama na watanzania kwa ujumla, Miradi imejengwa kwa vigezo stahiki kwa kipindi chote cha miaka minne ya utawala wake." aliongeza Mkuu wa Mkoa.
"Kwa mwaka 2020-2021 Chama cha Mapinduzi kimeahidi kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Ubungo wanajengewa barabara za ndani(barabara za mitaani) zenye urefu wa KM 111.76 ili kutatua kero ya barabara kwa wananchi hao" aliongeza Makonda.
Mkuu wa Mkoa alitoa taarifa ya ahadi ya Mhe. Rais aliyoahidi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya kuwa tayari fedha hizo zimeshaingizwa ili mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya uweze kukamilika.
Pia Mhe.Mkuu wa Mkoa alisema kuwa katika kuhakikisha anaendelea kuleta maendeleo kwa wananchi Mhe.Rais amesamehe riba ya mikopo inayotolewa na mfuko wa vijana, wanawake na watu wenye walemavu.
"Niwapongeze viongozi wa Wilaya ya Ubungo kwa mapokezi mazuri na tunaondoka tukiwa na matumaini mapya na mazuri na Wilaya ya Ubungo" alimalizia Mkuu wa Mkoa
NB. Ziara hii itafanyika kwa siku mbili kuanzia leo ambayo imefanyika kwa jimbo la Kibamba na kumalizika kesho tarehe 1/7/2020 kwa jimbo la Ubungo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa