Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla kwa kushirikiana na viongozi wa Wilaya ya Ubungo na wananchi wa Kata ya Manzese, ameshiriki zoezi la usafi wa mazingira na kutumia fursa hiyo kuwakumbusha wafanyabiashra kuwa zoezi la utoaji wa vitambulisho litafanyika kwa wale tu wanaofanya biashara kwenye maeneo rasmi pekee.
Makalla ametoa kauli hiyo wakati wa zoezi la usafi wa mazingira ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa kampeni ya Safisha, Pendezesha Dar es Salaam ambapo kimkoa hutekelezwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi huku Halmashauri ya Manispaa Ubungo ikitekeleza kila jumamosi.
Aidha, Makalla amesema kuwa mpango wa Serikali kwa machinga ni kuwapanga vizuri, kusafisha maeneo waliyotoka na kuboresha maeneo rasmi waliyopelekwa na kuyalinda maeneo waliyotoka ili yasivamiwe tena.
Makalla ametoa wito kwa wananchi wote kuwa kuna umuhimu wa kufanya usafi kwenye maeneo yao kila wakati ili dhana ya kupendezesha Jiji la Dar es salaam lionekane kwa vitendo kwani Dar es salaam ndiyo taswira ya Tanzania na Ubungo ni lango la Jiji.
Zoezi hili la usafi wa mazingira limehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mh Mstahiki Meya, Waheshimiwa Madiwani, Watendaji wa Kata na Mitaa, wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa