Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James amefungua rasmi tamasha la sensa Wilaya ya Ubungo Leo tarehe 20 agosti,2022 linalofanyika katika viwanja vya Barafu vilivyopo Mburahati
Aidha, Kheri ameutaarifu umma kuwa wananchi wote wa Wilaya ya Ubungo wako tayari kuhesabiwa
Aliendelea kwa kusema kuwa Viongozi wote wa vyama vya siasa niwaombe zoezi hili linaanza rasmi muwape ushirikiano makarani wa sensa wanaopita katika majumba yetu
Aidha, Kheri alisema kuwa zoezi la sensa lina maana kubwa sana kwa taifa, zinapopatikana Taarifa kamili za idadi ya wananchi waliopo inasaidia katika kupanga Mipango ya nchi na hasa mahitaji ya wananchi wake
Kheri Aliendelea kwa kusema kuwa kupitia sensa, miundombinu ya afya, elimu, barabara, maji n.k inaboreshwa, huduma za kijamii zinaendelea kupewa kipaumbele ili kukidhi mahitaji ya wananchi wake
Halikadhalika kwa Matukio mbalimbali yanaendelea ikiwemo burudani, michezo mbalimbali, wananchi wote mnakaribishwa
UBUNGO KUMENOGA MJE TUKESHE MPAKA MAJOGOO
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa